To read this content please select one of the options below:

Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia

Nanjala Nyabola (Nanjala Nyabola is an Independent Researcher based in London, UK)

Foresight

ISSN: 1463-6689

Article publication date: 13 October 2022

155

Abstract

Purpose

Maneno mengi yanayohusu haki za binadamu na haki za kiteknolojia hayajatafsiriwa katika lugha ya Kiswahili. Kwa hivyo, wataalamu wa teknolojia na watetezi wa haki za kidijitali hutumia maneno ya Kiingereza – hata bila utohozi – wanapozungumzia haki za kiteknolojia. Hali hii ya mambo inachangia udhoofu fulani katika utetezi wa haki za kidijitali kwani wanaojaribu kueleza jamii umuhimu wa haki hizi hulazimishwa kutegemea msamiati wa Kiingereza usiyo na msingi au viungo na lugha ya Kiswahili Katika makala hii, tutazungumzia umuhimu wa kukaribisha watu kutumia lugha za Kiafrika kwenye mtandao.

Design/methodology/approach

Kiswahili ni lugha ya Kiafrika inayozungumzwa katika eneo zaidi sana duniani. Karibu watu milioni mia moja na arobaini Afrika mashariki wanazungumza Kiswahili kama lugha yao ya kwanza au ya pili, miongoni mwao Wakenya na Watanzania, wenyeji wa nchi ambamo Kiswahili ni lugha ya kitaifa. Tena kuna historia ndefu ya kutumiwa kwa lugha ya Kiswahili katika uandishi, uchapishaji na ubunifu wa utamaduni wa kisasa. Kiswahili pekee yake ndiyo lugha ya asili ya Kiafrika inayotumika kama lugha ya maalum ya Umoja wa Mataifa za Kiafrika. Hata hivyo, kwa upande wa matumizi ya Kiswahili, hasa kwenye mada ya teknolojia, Kiswahili imewachwa nyuma.

Findings

Zaidi ya maneno rasmi, uwepo wa lugha za Kiafrika ni muhimu kuimarisha jumuiya za Kiafrika mtandaoni kwani lugha inalenga sana haki na utambulisho wa watu. Miradi za kutafsiri maneno za kiteknolojia katika lugha ya Kiswahili inahimiza jumuiya za Afrika Mashariki kuunda jamii inayosimamia matakwa yao vyema. Makala hii basi inazingatia umuhimu wa lugha kwenye kuunda jamii na katika hatua za kuondoa mbinu za kikoloni mtandaoni ili wenyeji wa Afrika Mashariki wajione mtandaoni kwa ujumla wao wote. Makala pia itazingatia semiotiki ya lugha katika ubunifu wa teknolojia, na umuhimu wa kutafsiri jamii ya lugha ya Kiswahili katika harakati za kuondoa ukoloni katika ubunifu huu. Lakini sio tu kwamba lugha ya Kiswahili ndio pekee inayoweza kuondoa mbinu za kikoloni mtandaoni, kwani pia lugha hiyo ina ishara za kutawalwa kwa jamii fulani. Bali makala hii inatumia mfano wa Kiswahili kuhimiza utumiaji wa lugha za kiasili au za kimama mtandaoni ili kulinda mustakabali wa kidijitali wa umma.

Originality/value

Umuhimu wa makala hii ni kuashiria jipya umuhimu wa lugha katika harakati za kuendeleza haki za kidijitali na hasa kuondoa mbinu za kikoloni kwenye teknolojia, swala lisilowahijadiliwa katika lugha ya Kiswahili.

Keywords

Acknowledgements

The English version of this paper was produced with support from the Africa Digital Rights Network.

Citation

Nyabola, N. (2022), "Uraia, Lugha na Haki za Kidijitali: umuhimu wa lugha katika harakati za kuondoa ukoloni katika teknolojia", Foresight, Vol. ahead-of-print No. ahead-of-print. https://doi.org/10.1108/FS-11-2021-0222

Publisher

:

Emerald Publishing Limited

Copyright © 2022, Emerald Publishing Limited

Related articles